Original article: How to Check if a JavaScript Array is Empty or Not with .length

Unapotengeneza programu katika JavaScript, unaweza kuhitaji kujua jinsi ya kuangalia ikiwa array ni tupu au la.

Ili kuangalia kama array ni tupu au la, unaweza kutumia sifa ya .length.

Sifa ya .length huweka au kurejesha idadi ya vipengele katika array. Kwa kujua idadi ya vipengee kwenye array, unaweza kujua ikiwa ni tupu au la. Array iliyo tupu itakuwa na vipengele 0 ndani yake.

Wacha tupitie mifano kadhaa.

Huu hapa ni Mfano Unaoonyesha Jinsi ya Kuangalia kama Array ya JavaScript ni Tupu au Sio kwa kutumia .length:

Mfano wa Sintaksia ya .length

Const myArray = [‘Horses’, ‘Dogs’, ‘Cats’];

Hapa tunaunda kiambajengo kuashiria array.

Kwe kutumia sifa ya .length, tunaweza kuangalia urefu wa array:

myArray.length

Hii itarudisha 3, kwa sababu kuna vitu 3 kwenye array.

Kuangalia kama array ni tupu au la kwa .length, tunaweza kufanya hivi kwa njia tatu.

.length mfano wa kwanza

Kwanza, hebu tuunde array mpya isiyo na vipengele.

const arr = []

Sasa tunaweza kuangalia kama array ni tupu kwa kutumia .length.

arr.length

Hii itarudisha 0, kwani kuna vitu 0 kwenye array.

.length mfano wa pili

Tunaweza pia kuangalia kwa hususani ikiwa array ni tupu au la.

if (arr.length === 0) { console.log("Array ni tupu!") }

Ikiwa array yetu ni tupu, ujumbe ulio hapo juu utaonyeshwa. Ikiwa array ina vipengee ndani yake, code iliyo ndani ya if block haitafanya kazi.

Hii hapa ni njia ya tatu ya kuangalia kama array ni tupu kwa kutumia .length.

.length mfano wa tatu

Kwa kuchanganya matumizi ya sifa ya .length na mantiki ya opereta ya "not" katika JavaScript ambayo ni ishara ya "!", tunaweza kuangalia kama array ni tupu au la.

Opereta ya “!” hukanusha usemi. Tunaweza kuitumia kurudisha true ikiwa array ni tupu.

Kwa mfano huu, hebu tufungue console yetu JavaScript. Ili kufungua console katika Chrome, unaweza kubofya Inspect -> Console.

Kwanza, tengeneza array bila vipengee ndani yake.

Array tupu

Kisha, tutumie opereta ya kimantiki ya “not”, pamoja na sifa yetu ya .length kuangalia kama array yetu ni tupu au la.

Not-Operator

Ikiwa hatungetumia opereta ya "not", arr.length ingerudisha 0. Opereta ikiwa imeongezwa, itarudisha true ikiwa uendeshaji wake ni false. Kwa sababu arr.length ni 0, au false, inarudisha true.

Wacha tuitumie hii na ujumbe wa if, na tuchapishe ujumbe ikiwa array yetu ni tupu.

Empty-Array

Wakati wa kuangalia ikiwa array ni tupu au la, mara nyingi ni bora kuangalia ikiwa array ni array kwa huakika.

kwa nini?

Kwa sababu kunaweza kuwa na wakati ulitarajia kuangalia urefu wa array, lakini badala yake unapewa aina tofauti ya data, kwa mfano, string:

string

Kwa sababu sifa ya length inaweza kutumika kwenye aina zingine za data, ni vizuri pia kuangalia ikiwa array yako ni array kama ulivyotarajia.

Ninapendekeza pia utumie njia ya Array.isArray() ili kuthibitisha array yako ni array kwa kweli. Njia hii huamua ikiwa kilichopitishwa ni array au la. Ikiwa kile kilichopitishwa kilikuwa array, njia hii itarudisha true.

Tuongeze njia hii kwa mfano wetu.

Jinsi ya kutumia njia ya Array.isArray()

Array.isArray

Hitimisho

Katika nakala hii, tulimefunza kutumia sifa ya length katika JavaScript kwa njia tofauti ili kuangalia ikiwa array ni tupu au la. Sifa ya urefu hurejesha idadi ya vitu katika array.

Pia tumejifunza kuwa ni vyema pia kutumia mbinu ya Array.isArray unapotumia sifa ya .length, ili kuangalia kama thamani iliyopitishwa ni array kama unavyotarajia.