Mwaka mmoja umepita tangu freeCodeCamp tufanye mwezi wetu wa kwanza wa tafsiri ulimwenguni mnamo Septemba 2021.
Sasa, ni Septemba tena - na hapa tuko kwa awamu ya pili ya tukio hili la mwezi mzima. freeCodeCamp tunaadhimisha mwezi wetu wa tafsiri ulimwenguni kwa mwaka wa pili mfululizo, unaofanyika Septemba 6 na kuendelea kwa mwezi uliosalia.
Mwezi wa Tafsiri ya Ulimwengu ni nini?
Mwezi wa tafsiri ulimwenguni ni mpango unaoendeshwa na freeCodeCamp ili kusaidia kutafsiri mtaala wa freeCodeCamp katika lugha nyingi za ulimwengu iwezekanavyo.
Tukio hili linakaribisha washirika wapya wa ujanibishaji na kuwashukuru wale ambao tayari wanasaidia katika mchakato wa kutafsiri.
Wakati wa hafla ya uzinduzi mwaka jana, freeCodeCamp ilifanya kipindi cha Twitter spaces. Katika kipindi hicho, tulizungumza na wachangiaji wetu na wale ambao wangependa kuanza kusaidia katika kutafsiri mtaala wa freeCodeCamp.
Rafael, kiongozi wa juhudi za utafsiri duniani kote, alitoa makala inayotangaza tukio hilo na kutoa baadhi ya data kuhusu juhudi za utafsiri hadi kufikia hapo.
Translation Progress to Date
Mengi sana yametokea katika miezi kumi na miwili tangu wakati huo. Tumepata wachangiaji kutoka lugha nyingi tofauti. Kwa mfano, kwa sasa mtaala mzima umetafsiriwa katika kiitaliano, kijapani, kireno, na kiukreni.
Wengine wameanza mchakato wa kutafsiri vyeti vitatu vya msingi - Muundo wa Wavuti Unaoitikia (katika toleo lake la hivi punde), JavaScript, na Maktaba za Front-End - kama vile kiarabu, kibengali, kifaransa, kijerumani, kiindonesia, kikorea, kiajemi, kiromania, kirusi, kituruki, na kiurdu.
fCC’s certifications translated to Italian and Japanese (above), Portuguese and Ukranian (below).
Jumuiya pia tumebadilisha mtazamo wetu kidogo. Mwaka huu, tulifanya uamuzi wa kuelekeza umakini wetu kwenye uchapishaji wa freeCodeCamp na tukaanza kutafsiri makala kwa lugha zingine za ulimwengu.
Hilo limefanya kutolewa kwa sehemu ya uchapishaji wa tovuti hiyo katika lugha nyingi. Wahispania na wachina wanaendelea na kazi yao ya kushangaza, na sasa tuna zaidi ya makala 475 katika kihispania na zaidi ya makala 1,000 katika kichina.
Kireno kina takriban makala 350 na kiitaliano kina zaidi ya makala 200 zilizotafsiriwa. Sehemu za habari za kijapani, kibengali, kiarabu, na kiurdu pia zimekuwa zikitoa tafsiri nyingi zaidi za machapisho yao.
Hii haimaanishi kwamba tunaacha mtaala nyuma. Kazi zote mbili zinafanyika kwa wakati mmoja, wachangiaji wakisaidia katika mtaala huku wengine wakisaidia katika utafsiri wa makala.
Baadhi ya wachangiaji husaidia katika nyanja zote mbili, kutafsiri makala na mtaala katika muda wao wa ziada.
Mabadiliko katika Idhaa Zetu za Mawasiliano
Pia tumebadilisha jinsi tunavyowasiliana na washirika wetu wa ujanibishaji. Mnamo Juni, tulihamisha vyumba vyetu vya gumzo tunavyotumia kuwasiliana na washirika wetu hadi kwenye seva ya Discord.
Hii ilifanya iwe rahisi kutagusana na wachangiaji. Pia imewasaidia kutagusana kwa urahisi zaidi wao kwa wao na vilevile na wanajamii wengine ambao wanajifunza kusimba.
Vyumba vya gumzo kwa tafsiri/ujanibishaji viko chini ya Ujanibishaji, kama unavyoona kwenye picha.
Localization chat rooms on the fCC Discord server
Iwapo campers wanahitaji usaidizi wa mtaala kwa ujumla, bado wanauliza maswali kwenye forum ya FreeCodeCamp.
Pia tumeweka sehemu katika lugha tofauti kwenye forum ili kuwasaidia watu ambao wana shaka wakati wa safari yao katika mtaala lakini wanaona vigumu kuuliza maswali yao kwa Kiingereza.
Several localized sections of the fCC forum are now available
Kusudi la Mwezi wa Tafsiri Ulimwenguni
Madhumuni ya Mwezi wa Tafsiri ya Ulimwengu ni mambo mawili:
- kuwashukuru wachangiaji wetu kwa yote ambayo wamekuwa wakifanya ili kutusaidia kuleta mtaala na uchapishaji wa freeCodeCamp kwa lugha nyingi za ulimwengu iwezekanavyo, na
- kuwaalika washirika zaidi kuwa sehemu ya juhudi zetu za kutafsiri.
Quincy alichapisha makala mnamo Juni ambapo unaweza kusoma kuhusu jinsi ya kuwasiliana nasi ili kutoa usaidizi wa utafsiri.
Tungependa pia kuonyesha shukrani zetu kwa washirika wetu ambao wamechukua muda wao kutoa maandishi zaidi na zaidi katika lugha zao. Mitaala na makala haya yaliyotafsiriwa huwawezesha watu ulimwenguni kote kujifunza kusimba katika lugha zao za asili.
Nishani za Mwezi wa Tafsiri Ulimwenguni
Mwaka huu, kwa mara nyingine tena tutatoa nishani kwa wachangiaji ambao wametusaidia kutafsiri makala za uchapishaji mwezi mzima. Ingawa makala zinaweza kutofautiana kwa ukubwa, tunaelewa kwamba kila moja inahitaji jitihada nyingi.
Kutafsiri makala ni tofauti kabisa na kutafsiri mtaala. Washiriki wanaweza kutafsiri utungo mchache katika mtaala na kuacha kuchangia. Lakini kila mchangiaji anawajibika kwa makala nzima mara tu anapoamua kuitafsiri. Kwa hivyo washiriki huanza na kumalizia tafsiri ya makala wanayochagua, kitu ambacho wanafanya vyema.
Wakati wa tukio la mwezi wa tafsiri ulimwenguni, tutawapa washiriki wote ambao wameshirikiana mwaka mzima nishani ya mwezi wa tafsiri ulimwenguni.
Pia, mwishoni mwa tukio, tutawasilisha nishani maalumu kwa watafsiri wajuu zaidi ambao wametoa michango mingi zaidi katika mwezi wa Septemba.
Utaweza kuonyesha nishani hizi kwenye mtaala wako wa freeCodeCamp na wasifu wa forum ikiwa ungependa kufanya hivyo.
Asante kwa Wafasiri, Wachangiaji na Wasomaji Sahihi Wote!
Iwapo ungependa kusaidia kutafsiri mtaala wa freeCodeCamp katika lugha yoyote ya ulimwengu, tembelea kituo cha wachangiaji wetu kwenye Discord, na usome makala ya Quincy kuhusu jinsi ya kuchangia na kujifunza zaidi.
Ikiwa wewe ni sehemu ya mpango huu na umechangia kwa kujitolea kuleta rasilimali nyingi za freeCodeCamp kwa lugha yako ya asili, asante! Tunatoa shukrani zetu za dhati na tunatumai kwamba mchakato umekusaidia kujifunza na umekuwa wa kufurahisha kwako. Endelea na kazi nzuri!
Tungependa kusikia mawazo au maoni yako kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha uzoefu wako na machapisho ya Kiswahili!
Tafadhali jaza utafiti huu wa haraka na utujulishe mawazo yako